pmbet

Waomba hifadhi Uingereza sasa kupelekwa Rwanda, Bunge laidhinisha

Eric Buyanza

April 23, 2024
Share :

Mpango wenye utata wa serikali ya Uingereza wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda hatimaye umeidhinishwa na Bunge. 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya vuta ni kuvute iliyodumu hadi usiku wa manane kati ya baraza la juu la bunge la Uingereza House of Lords na baraza la House of Commons.    

Wajumbe wa baraza hilo la juu, ambao hutathmini sheria iliyopendekezwa, waliurejesha mara kadhaa muswada huo kwa marekebisho lakini hatimaye waliafiki na hilo linamaanisha muswada huo sasa utakuwa sheria. 

Kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, ni sehemu muhimu ya majibu ya Waziri Mkuu Sunak katika kukomesha vitendo vya waomba hifadhi kuingia kinyume cha sheria nchini Uingereza. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet