Wapanda mahindi kwa mfano wa sura ya Messi
Eric Buyanza
June 19, 2024
Share :
Mwaka 2023 zaidi ya wakulima ishirini wa Argentina na mashabiki wakubwa wa gwiji wa soka Lionel Messi, walipanda mahindi kwenye mashamba yao kwa kufuata mfano wa sura ya mchezaji huyo maarufu ikiwa ni asante ya kufanikisha nchi yao kutwaa kombe la dunia lililofanyika nchini Quatar na kutamatika December 18, 2022.
Ili kufanikisha hilo, wakulima hao walipanda mahindi wakitumia kanuni ya kilimo waliyopewa na mhandisi wa kilimo aliyefahamika kwa jina la Carlos Faricelli.
Lionel Messi ana mamilioni ya mashabiki duniani kote, lakini hakuna mahali anapopendwa zaidi kama nyumbani kwao Argentina, ambako watu wengi wanamwona kuwa mungu wa soka.