Wapinzani wa Simba, Yanga wakimbia Mapinduzi Cup
Sisti Herman
December 25, 2023
Share :
Kamati ya Michuano ya Mapinduzi Cup 2024, kupitia Mwenyekiti wake Mbarouk Othman ametangaza mabadiliko ya Timu mbili zilizopangwa kushiriki mashindano hayo kwa msimu huu kutokana kujitoa kwa Timu ya Bandari ya Kenya na URA ya Uganda.
Mwenyekiti wa kamati hio amesema kutokana na sababu mbali mbali, Timu ya Bandari na URA zimejitoa katika mashindano hayo na nafasi zao zitachukuliwa na JKU SC ya Unguja na JAMUS ya Sudani Kusini.
Kupitia Taarifa hiyo, Kamati imelazimika kufanya mabadiliko ya Makundi pamoja na ratiba kwa ujumla na kwa sasa makundi yamepangwa kama ifuatavyo:-
Kundi 'A'
Azam FC, Vitalo'o, Chipukizi na Mlandege
Kundi 'B'
Simba SC, APR, Singida FG na JKU
Kundi 'C'
Yanga SC, Jamhuri, KVZ na Jamus.
Bingwa wa michuano atachukuwa kitita cha Shilingi Milioni Mia Moja (Milioni 100) na Mshindi wa pili ni Shilingi Milioni Sabini (Milioni 70).
Michuano itaanza Disemba 28, 2023 katika Uwanja wa Amaan kwa Unguja na Gombani kwa Pemba.
Viingilio vya michezo ya Mapinduzi Cup .
Mechi zitakazochezwa Saa 10:15 jioni, Kiingilio ni Shilingi 5000 Wings na 3000 Mzunguko.
Mechi zitakazochezwa Saa 2:15 usiku Kiingilio Wings 10000, Jukwaa la Mashariki (Urusi) 5000 na Jukwaa la Kusini na Kaskazini 3000.
Eneo la V.I.P litakuwa na tiketi maalum na Idadi ya watu maalum.