pmbet

Wapinzani wa Singida Black Stars Kagame Cup hawa hapa

Sisti Herman

August 28, 2025
Share :

 

Wawakilishi wa Ligi kuu Tanzania bara kwenye Kombe la shirikisho Afrika Singida Black Stars wamepangwa Kundi A pamoja na Garde Cotes FC (Djibouti), Ethiopia Coffee SC (Ethiopia) na Kenya Police FC katika hatua ya makundi ya michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025 Katika droo iliyochezeshwa Alhamisi asubuhi kwenye Pan Pacific Suites jijini Nairobi.

Michuano hiyo yenye timu 12 itafanyika Septemba 2-15 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mashindano ya CECAFA aliyechezesha droo hiyo, Yusuf Mossi alisema mashindano hayo yatafanyika katika viwanja vya Azam Complex, Chamazi, KMC na Meja Jenerali Isamuyo.

"Mashindano haya pia yatasaidia timu zetu za ukanda huu kujiandaa kabla ya mashindano ya CAF ya 2025/2026 ambayo yataanza mwezi ujao," Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA Auka Gecheo alisema.

Al Hilal, ambao pia wataiwakilisha Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika wamepangwa Kundi C pamoja na Kator FC (Sudan Kusini), Mogadishu City Club FC (Somalia) na Alahly SC Wad Madani (Sudan).

Kundi A: Singida Black Stars FC, Garde Cotes FC, Ethiopian Coffee SC, Kenya Police FC

Kundi B: APR FC, NEC FC, Bumamuru FC, Mlandege FC

Kundi C: Al Hilal, Kator FC, Mogadishu City Club, Alahly SC Wad Madani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet