pmbet

Wapinzani wateuliwa baraza jipya la Mawaziri Kenya.

Joyce Shedrack

July 24, 2024
Share :

Rais wa Kenya Wiliam Ruto ametangaza Baraza jipya la mawaziri akiwajumuisha baadhi ya wanasiasa wa mrengo wa upinzani akiwemo aliyekuwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho aliyemteuwa kuwa Waziri wa Madini huku John Mbadi akipewa Wizara ya Fedha.

Rais Ruto ametangaza baraza hilo leo Julai 24, 2024 zikiwa zimepita siku chache tangu atangaze orodha ya kwanza ya majina kumi Ijumaa Julai 19 mwaka huu akiwarudisha sita waliokuwa mawaziri katika baraza alilovunja jambo lililosababisha baadhi ya Gen Z kuhitisha maandamano mengine siku ya jana kupinga majina sita yaliyorudishwa.

Mawaziri wapya 10 walioteuliwa leo kuunda baraza la Mawaziri 20 ni John Mbadi kuwa Waziri wa  Fedha, Salim Mvurya  Waziri wa Viwanda na Uwekezaji
Rebecca Miano Waziri wa Utalii, James Wandayi Waziri wa Nishati ,Kipchumba Murkomen  Waziri wa Vijana na Michezo,Hassam Joho Waziri wa Madini, Alfred Mutua Waziri wa Kazi na Hifadhi ya Jamii, Wycliffe Oparanya  Waziri wa Maendeleo ya Ushirika wa Biashara zinazochipukia, na za Kati,Justin Muturi Waziri wa Utumishi wa Umma na Ufanisi na Stella Soi Lang’at  Waziri wa Masuala ya Jinsia.

Mabadiliko hayo yanafanyika kufuatia maandamano ya wiki kadhaa kwa vijana wa nchi hiyo maarufu Gen Z waliokuwa wakipinga Serikali ya Rais William Ruto huku wakishinikiza mabadiliko.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet