Warembo walalamika kukosa wanaume kisa michoro ya 'Tattoo'
Eric Buyanza
April 11, 2024
Share :
Baadhi ya warembo waliojichora Tattoo za kudumu (zisizofutika) wanalalamika kuwa wanatengwa na wanaume.
Chanzo chetu kimekutana na baadhi yao ambapo mmoja amesema imekuwa vigumu kwao kupata wanaume wa kudumu nao kwenye mahusiano, kwasababu wanaume wamekuwa wakiwakwepa bila sababu za msingi.
“Siamini licha ya urembo wangu sijapata mwanaume wa kunipenda eti kwa sababu tu nimejichora tattoo,” akashangaa mwanadada huyo aliyejitambulisha kwa jina la Asha.
Kwa mujibu wa Asha alijichora Tattoo yake ya kwanza alipokuwa Chuo Kikuu baada ya kushawishiwa na wenzake, na alifanya hivyo kwa kuamini Tattoo ni urembo kama ulivyo urembo mwingine wowote.
Hata hivyo kwa upande mwingine anaonyesha kujutia maamuzi yake kwa sababu alijichora Tattoo ambazo haziwezi kufutika maishani.
“Ninatamani kuwa kwenye mahusiano na mwanamume mmoja tu wa kunipenda kwa dhati, lakini inakuwa vigumu kwa sababu wale ambao wamenitokea huniacha siku chache tu kabla hata mahusiano hayajaanza kunoga,” analalamika Asha.
Naye mrembo mwingine akitoa ushauri kwa wanaume kuhusu jambo hilo amesema;
“Ningependa kuwashauri wanaume kuangalia zaidi tabia za wanawake badala ya kuwabagua kwa michoro waliyonayo mwilini,”