pmbet

Warioba aitaka serikali kurekebisha kasoro za uchaguzi Serikali za Mitaa.

Joyce Shedrack

December 4, 2024
Share :

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba ameitaka Serikali irekebishe kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu, ili zisijitokeze kwenye uchaguzi mkuu wa Urais, Wabunge na Madiwani mwaka 2025.

Jaji Warioba amemtaka Rais kusimamia 4R, lakini pia amewataka wanasiasa kufata utashi wa Taifa na si kusimamia maslahi ya vyama vyao, lakini pia akitaka jeshi la Polisi lisihusishwe kwenye Siasa.

Akizungumzia utekaji na mauaji yaliyojitokeza Mzee Warioba amesema si vyama vya upinzani tu hata CCM pia liliwaathiri hivyo ametaka Jeshi la Polisi kuthibiti hali hiyo na pia amepongeza juhudi zilizofanyika hadi sasa katika kukamata watu hao.

" Watanzania tusitazamane kama Chama " Sasa hivi hatuna Amani kuna watu wanaogopa".Alisema Mzee Warioba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet