pmbet

Warusi wawasili kuonesha njia za kupambana na uhalifu

Eric Buyanza

April 29, 2024
Share :

Wataalam kutoka Ofisi kuu ya Waendesha Mashtaka nchini Urusi, wamewasili nchini kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kitaaluma litakaofanyika tarehe 30 Aprili 2024 katika shule ya uanasheria kwa vitendo Tanzania ( Law School) Jijini Dar es Salaam.

Katika kongamano hilo watalaam hao watatoa mada tatu ikiwa ni pamoja na kueleza namna ambavyo Wanasheria wa Shirikisho la Urusi wanavyofanya kazi, Utaalam na uzoefu wao katika kupambana na matukio ya uhalifu wa Kimataifa.

Prof. Ambrose Kessy kutoka Shule ya Sheria Tanzania (Law School), amebainisha hayo alipowapokea watalaam hao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet