pmbet

Wasanii achananeni na 'Kiki' tukuze muziki wetu - Sky

Joyce Shedrack

March 11, 2024
Share :

Mkongwe kunako tasnia ya habari,  Fredrick Bundala almaarufu kwa jina la ‘SKY’ amewataka wasanii wa muziki wa hapa Bongo kuachana na kiki ili kuweza kuusaidia muziki wa Tanzania kukua zaidi kimataifa kama ilivyo kwa wasanii wa Nigeria.
 

“Bifu ni mbaya kwa sababu uadui wa hizi timu mbili kati ya Diamond na Alikiba wakiingia kwenye malumbano soko linakuwa liawazingatia wao peke yao, mashabiki wanashindwa kuwapokea wasanii wapya…..naamini muziki mzuri na kufanya connection nzuri ndio njia nzuri ya kuupaisha muziki wetu” amesema SKY.
 

SKY amesema ili kukuza muziki wa Tanzania ni lazima jitihada ziongezeke na kuwekeza zaidi kwa wasanii chipukizi, kwani collabo pekee sio kitu kitakachoweza kumsaidia msanii mdogo kukua kimataifa.
 

Pia ametoa ushauri kwa wasanii wa Afrika Mashariki kushirikiana ili kushindana na wasanii wa Nigeria, badala ya kuanza kupigana vijembe wenyewe kwa wenyewe kwani hilo halitasaidia chochote.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet