Wasanii wa Tanzania watikisa Kenya Zuchu kinara.
Joyce Shedrack
January 9, 2025
Share :
Wasanii wa Tanzania wanaongoza kufatiliwa zaidi nchini Kenya kwa kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube huku 5 bora wote wakiwa ni wasanii wa bongofleva kutokea hapa 255 Tanzania.
Hii inaonyesha bongofleva inamashabiki wengi zaidi kutoka za Nchini Kenya na wasanii wake kwanza alafu wengine ndio wanafata.
Katika orodha hiyo Msanii anayeongoza ni malkia wa WCB Zuchu huku namba mbili akiwa ni Simba la Masimba Diamond Platnumz,namba tatu ni Konde Boy Harmonize,namba 4 ni Chui Rayvanny na namba tano akiwa ni Marioo.