pmbet

Wasanii wenye vipaji Nigeria hatufiki watano - Ruger

Eric Buyanza

November 7, 2024
Share :

Mwanamuziki wa Afrobeats, Michael Adebayo Olayinka almaarufu kwa jina la 'Ruger' ameeleza masikitiko yake kuhusu wasanii wasio na vipaji kupata umaarufu katika tasnia ya muziki nchini Nigeria kutokana na prmotion kubwa wanayopata.

Ruger anasema hali hiyo imekuwa ikimuumiza kwa sababu, hata wasanii wasio na vipaji wanaweza kupata umaarufu ikiwa tu wana pesa za kufanya promotion.

Siku kadhaa zilizopita Ruger alikaririwa akisema Nigeria kwa sasa ina wanamuziki wasiozidi watano wenye vipaji.

Akizungumza jijini Lagos katika mahojiano na Cool FM, Ruger alisema wale ambao wana vipaji na wanaofanya muziki mzuri hawafiki watano.

"Mimi sio msanii mkubwa Nigeria, lakini ukizungumzia wenye vipaji, niko mahali flani na hatujafika watano,” alijitapa Ruger.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet