Washirika waanza kumtema Diddy
Eric Buyanza
December 12, 2023
Share :
Imeripotiwa takribani kampuni 18 zimesitisha uhusiano wao wa kibiashara na kampuni ya Rapa Sean Combs "P Diddy" ijulikanayo kama "Empower Global" kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili.
"Tumepatwa na shuruti la kimaadili kusitisha uhusiano wetu" - kampuni moja ilitamka dhidi ya "Empower Global"
Kwa mujibu wa jarida la Rolling stone, kampuni 18 zimetemana na P diddy baada ya tuhuma zake za unyanyasaji wa kingono kushika kasi .
"Hatuwezi na Hatutoweza ku-sapoti unyanyasaji kwa wanawake" - Mmiliki mmoja wa kampuni aliiambia Rolling stone.