pmbet

Wasomi msifungie elimu na tafiti zenu ndani

Eric Buyanza

December 29, 2023
Share :

Serikali imewataka wahitimu wa vyuo mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa hawafungii matokeo ya Tafiti zao na badala yake watumie matokeo ya Tafiti lakini pia elimu zao Katika kuleta matokeo chanya ndani ya Jamii.

Endapo kama kila muhitimu wa ngazi mbalimbali ya elimu ataweza kutumia ipasavyo ujuzi alioupata itaweza kuiraisishia Jamii kuepukana na changamoto mbalimbali.

Hayo yameelezwa Arusha na Naibu waziri wa kilimo David Silinde Wakati akiwatunuku vyeti wahitimu kutoka katika chuo cha uasibu Arusha kwenye maafali ya 25 ambayo yalifanyika katika hoteli ya Ngurdoto.

Waziri Silinde alisema kuwa matokeo ambayo yanatolewa na watafiti ambao wameitimu vyuo vikuu ni mazuri Kwa kuwa yanakuja Kabisa na Majibu hasa Yale ambayo yanaikabili Jamii.

“Nawasihi sana wasomi hakikisheni kuwa hamhifadhi Elimu ambazo mmezipata na badala yake njooni na majibu juu ya changamoto mbalimbali ambazo bado zinaitesa jamii yetu ya kitanzania toeni majibu kwa serikali Lakini pia hata Kwa sekta bonafsi “aliongeza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet