pmbet

Wataalamu wa uchambuzi wa PMTV washiriki mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa Barcelona

Sisti Herman

April 24, 2026
Share :

 

Wataalamu wa uchambuzi wa kipindi cha Pre and Post Match Analysis cha PMTV Tanzania, Sisti Martin ‘Sistiinho’ na Raymond Elias Mwaikamila wameshiriki mafunzo ya Sayansi na teknolojia ya uchambuzi wa mchezo wa mpira wa miguu yaliyoendeshwa na taasisi ya kimataifa ya Hudl inayojihusisha na teknolojia ya sayansi ya mpira wa miguu kwenye uchambuzi wa mechi, utunzaji na usimamizi wa takwimu za mchezaji mmoja mmoja na timu.

 

 

Kwenye mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Degigo Sports Management ambao wana leseni ya kuandaa matukio inayotambuliwa na shirikisho la soka nchini (TFF) kupitia wakala wake Hadji Degigo, kati ya mada zilizofundishwa ni pamoja na namna ya kutumia teknolojia ya Hudl kwenye uchambuzi wa kabla ya mchezo, wakati wa mchezo na baada ya mchezo kuanzia kwa mchezaji mmoja mmoja hadi timu kwa ujumla kwa kuangalia masuala ya kimbinu, kiufundi na utimamu wa miili ya wachezaji.

 

 

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye hotel ya Urbun Hotel by City Blue Masaki jijini Dar es Salaam yamehudhuriwa na wataalamu wa uchambuzi kutoka timu mbalimbali za Tanzania kama Faraji Muya wa JKT Tanzania, Bertha Kazobe wa JKT Queens na Timu za Taifa za wanawake, Martin Hummels wa Tausi FC ya ligi ya wanawake na wataalamu wa uchambuzi kutoka vyombo vingine vya habari kama George Ambangile wa Wasafi Media, Salum Pelembo wa Magic FM, Hadji Degigo wa Azam Media na wengine wengi.

 

 

Mafunzo hayo yameendeshwa na wataalamu na wakufunzi wa kimataifa kutoka Barcelona nchini Hispania Irene Martinez Villalonga na Federica De Peron kutoka Hudl chini ya usimamizi wa Degigo Sports Management chini ya Hadji Degigo

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet