pmbet

Wataka ngoma ya 'Kanga moja' ipigwe marufuku Zanzibar

Eric Buyanza

May 15, 2026
Share :

Mwakilishi wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub, ametaka serikali Zanzibar kupiga marufuku baadhi ya ngoma zenye viashiria vya kwenda kinyume na maadili, ikitolea mfano ya kanga moja kwamba ni miongoni mwa zinazochangia mmomonyoko wa maadili visiwani humo.
 

Mwakilishi huyo ametoa kauli hiyo leo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani, wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

 

Jaku amesema ngoma hiyo imekuwa ikihusisha mitindo ya uchezaji na mavazi yasiyoendana na utamaduni wa Kizanzibar, hali ambayo ni hatari kwa malezi ya watoto na vijana.
 

"Zanzibar ina historia na utamaduni wa kipekee unaopaswa kulindwa kwa nguvu zote, burudani yoyote inayokwenda kinyume na maadili ya dini na mila za wananchi haipaswi kupewa nafasi," amesema.
 

Ameongeza kuwa ni wajibu wa serikali kupitia mamlaka husika kuhakikisha burudani hiyo inafuatiliwa kwa karibu ili kuzuia maonyesho yanayoweza kuathiri maadili ya jamii.

 

Kauli ya Jaku imezua kicheko ndani ya ukumbi wa baraza hilo baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zuberi Ali Maulid, kushangazwa na jinsi mwakilishi huyo alivyoifahamu kwa undani ngoma ya kanga moja, hali iliyowafanya wajumbe wengine kuangua vicheko.
 

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet