pmbet

Watakaorithi mikoba ya kocha wa Chelsea watajwa

Eric Buyanza

April 22, 2026
Share :

Warithi watarajiwa wa Liam Rosenior pale Stamford Bridge wametambuliwa.

Hili linajiri baada ya kichapo cha 3-0 dhidi ya Brighton Jumanne usiku, ambapo wengi wa mashabiki wa Chelsea walionyesha hamu yao ya kutaka Liam Rosenior atimuliwe kazi.

 

Chelsea sasa imeporomoka hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa nyuma ya Liverpool inayoshika nafasi ya tano kwa pointi saba, jambo ambalo linapunguza kwa kiasi kikubwa nafasi yao ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

 

Hata hivyo, ikiwa kocha Rosenior atashindwa kuimarisha uchezaji wa kikosi chake basi ni dhahiri kutakuwa na shinikizo kubwa zaidi kutoka kwa mashabiki la kutaka afukuzwe.

 

Licha ya kiwango duni cha Chelsea katika Ligi ya Premia, timu ya Rosenior ina nafasi ya kutinga fainali ya Kombe la FA msimu huu, huku ikipangwa kukutana na Leeds United katika nusu-fainali huko Wembley Jumapili.

 

Kulingana na taarifa zilizosambaa kwenye korido za Stamford Bridge, mbrazil Filipe Luis, Cesc Fabregas ambaye anaifundisha klabu ya Como ya Serie A na Oliver Glasner ambaye ataondoka Crystal Palace mwishoni mwa msimu.

 

Wengine ni Xavi Hernandez, Roberto De Zerbi, Marco Silva, Unai Emery, Andoni Iraola, Frank Lampard, Fabian Hurzeler, Luis Enrique, Xabi Alonso, na Julian Nagelsmann.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet