pmbet

Watakaovujisha siri za jeshi wapigwe risasi - Trump

Eric Buyanza

October 15, 2026
Share :

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa watu wanaovujisha taarifa za operesheni za kijeshi kwa vyombo vya habari wanapaswa kupigwa risasi.

Trump alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kampeni huko Arizona, akionesha hasira zake kufuatia taarifa zilizovuja kuhusu muda wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran yaliyofanyika mwaka jana.

 

Rais huyo  alisema uvujishaji wa siri za kijeshi ni kosa kubwa, akidai kuwa katika nyakati zilizopita watu waliokuwa wakifanya hivyo waliadhibiwa vikali zaidi.

Matamshi hayo yanakuja wakati mjadala kuhusu adhabu ya kifo ukiendelea nchini Marekani.

 

Wizara ya Ulinzi ya Marekani inapanga kutekeleza hukumu ya kwanza ya kifo kwa mwanajeshi katika kipindi cha miaka 65 ijayo mwezi Desemba mwaka huu.

Kauli ya Trump imeibua mjadala mpya kuhusu usalama wa taarifa za serikali na mipaka ya adhabu kwa wanaovujisha siri za taifa nchini Marekani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet