pmbet

Watalii kulala kwenye bustani za Clock Tower katikati ya Jiji la Arusha.

Joyce Shedrack

March 6, 2025
Share :

Kuelekea Kilele cha siku ya wanawake duniani, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, ametambulisha sehemu mpya ya malazi na vyumba vya kulala wageni, vinavyopatikana kwenye bustani ya mzunguko wa Barabara ya Mnara wa saa 'Clock tower' .

Eneo hilo litatumika kuwapokelea watalii na watu mbalimbali kwenye eneo hilo kabla ya kuelekea kwenye maeneo ya Utalii. 

 

Mhe. Makonda amekuwa akihamasisha umuhimu wa wananchi wa Arusha kubuni vivutio na bunifu mbalimbali katikati ya Jiji hilo la kitalii vitakavyochochea na kuinua kiwango cha matumizi ya fedha kwa wageni na watalii wanaofika Mkoani hapa katika jitihada za kukuza uchumi wao binafsi na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet