Watano wafariki baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka
Eric Buyanza
May 25, 2024
Share :
Watu wasiopungua watano wamekufa na wengine kadhaa haijulikani walipo baada ya maporomoko kutokea kwenye mgodi wa dhahabu usio rasmi kaskazini mwa Kenya.
Watu wawili waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu hospitalini. Kamishna wa Kaunti ya Marsabit David Saruni amesema ajali hiyo imesababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Kiongozi wa serikali kwenye eneo hilo, Paul Rotich amesema ripoti kutoka kwa vikosi vya uokoaji, imebaini kuwa wachimbaji 8 walikuwa ndani ya mgodi huo wakati maporomoko hayo yanatokea.