pmbet

Watano wafariki kwa ajali Arusha

Sisti Herman

March 17, 2024
Share :

Watu watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha daladala kugongana na lori la magogo katika Mji Mdogo wa Ngaramtoni wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha.

Ajali hiyo imetokea jana Jumamosi Machi 16, 2024 saa 2:30 usiku ikiwa zimepita siku 22 tu tangu kutokea ajali nyingine iliyohusisha magari matatu katika mji huo wa Ngaramtoni iliyotokea Februari 24, 2024 na kuua watu 25 na kujeruhi wengine zaidi ya 21.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema kuwa miili yote mitano ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Seliani na majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

"Chanzo halisi cha ajali hiyo haijafahamika lakini kwa awali ni uzembe wa dereva la lori kupaki njiani, hivyo tunaendelea kumtafuta tukisubiri dereva wa daladala apate nafuu kwa kuwa ni mmoja wa majeruhi," amesema Kamanda Masejo.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet