pmbet

Watanzania wakamatwa na dawa za kulevya za Tsh Bil. 73

Sisti Herman

November 9, 2026
Share :

 

Polisi nchini Kenya wamewakamata raia wawili wa Tanzania na mwanamke mmoja raia wa Uganda katika operesheni ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya iliyofanyika katika Kaunti ya Kwale.

Katika operesheni hiyo, mamlaka zimefanikiwa kukamata kilogramu 454 za dawa zinazodhaniwa kuwa ni methamphetamine, zenye thamani ya takribani shilingi bilioni 3.6 za Kenya kwa bei ya soko la magendo.

Kwa mujibu wa Radio 47 Kenya, dawa hizo za kulevya zilikamatwa Novemba 8, 2026, huku raia hao watatu wa kigeni wakitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhusika na usafirishaji wa dawa hizo.

Tukio hilo linaelezwa kuwa ni moja ya mafanikio makubwa katika operesheni za kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Kenya, kutokana na kiasi kikubwa cha dawa zilizokamatwa pamoja na thamani yake.

Hata hivyo, mamlaka za Kenya bado hazijatoa taarifa zaidi kuhusu utambulisho wa washukiwa hao, chanzo cha dawa hizo za kulevya, pamoja na mazingira yaliyosababisha kukamatwa kwao.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi kuhusiana na tuhuma zinazowakabili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet