Watanzania waungana kumtakia Mzee mwinyi uponyaji wa haraka
Eric Buyanza
February 3, 2024
Share :
Siku moja baada ya kutolewa taarifa ya kuugua kwa Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, viongozi na watu mbalimbali wamemtakia afya njema kiongozi huyo mstaafu.
Taarifa ya kuugua kwa kiongozi huyo ilitolewa jana usiku Februari 2, 2024 na Msemaji wa familia, Abdulla Ali Mwinyi aliyesema kiongozi huyo amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua hivyo kutokana na ushauri wa daktari familia imeona ni vema apate faragha akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.
PMTV tunaungana na watanzania wote kumuombea uponyaji wa haraka, Mzee wetu Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Tanzania.