pmbet

Watatu waenda jela maisha kwa kumbaka mwanamke mkoani Dodoma

Eric Buyanza

June 4, 2026
Share :

Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imewahukumu William Chilenga (25), Masafa Mwaluganje (19) na Aman Leonard (25) kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la ubakaji wa kundi.

 

Washtakiwa walitenda kosa hilo Desemba 12, 2025 katika Kijiji cha Hombolo, Wilaya ya Mtumba mkoani Dodoma, ambapo walimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 42.

 

Baada ya tukio hilo, walikamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Hukumu hiyo ilitolewa Juni 2, 2026 na Hakimu Mfawidhi Lugoye baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka na kuwatiwa hatiani kwa kosa hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet