Wateteaji haki za mashoga, wanyimwa usajili wa kampuni
Eric Buyanza
March 13, 2024
Share :
Mahakama nchini Uganda imetupilia mbali ombi la kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja la Sexual Minorities Uganda (SMUG) linalotaka kupata usajili nchini humo.
Mahakama hiyo imesema usajili wowote wa kundi hilo ni kinyume na sera za nchi hiyo.
Walalamikaji walikuwa wanataka kusajili SMUG kama kampuni ili kuiwezesha kufanya kazi kihahali nchini Uganda, nchi ambayo imeharamisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.