pmbet

Watoto 194 wapewa mimba ndani ya mwezi mmoja

Eric Buyanza

May 17, 2024
Share :

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amesema kuwa ndani ya mwezi mmoja jumla ya watoto 194, wakiwemo wanafunzi katika Wilaya ya Momba wamepewa mimba.

Kufuatia hali hiyo ametoa siku 21 kwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenani Kihongosi  kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha watu wote waliohusika na vitendo hivyo wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kwenye hili hatuna masihara hata kidogo na Mkuu wa Wilaya nataka hawa waliongiza mimba kwa hawa watoto 194 tuone nao wanaingizwa kwenye vyombo vya sheria na baada ya siku 21 nataka nipate majibu mmefika wapi, hatuwezi kuleana na mambo ya namna hii”.
TM

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet