pmbet

Watoto 6 wafariki baada ya basi la shule kugongana na treni

Eric Buyanza

August 1, 2024
Share :

Watoto sita walifariki jana Jumatano jioni baada ya treni kugongana na basi la shule nchini Afrika Kusini, na kujeruhi wengine 20, wizara ya uchukuzi ilisema katika taarifa.

VOA imeripoti kuwa ajali hiyo ilitokea karibu na kijiji cha Mafube, umbali wa kilomita 180 kutoka jiji la Johannesburg.

Akiongea na wanahabari, Naibu waziri wa uchukuzi Mkhuleto Hlengwa alinukuliwa akisema;

β€œUsalama wa watoto wetu ni wa muhimu na ni jambo la kushtushasana kushuhudia maafa kama haya.”

Polisi waliripoti kwamba dereva wa basi hilo alitoroka eneo la tukio baada ya ajali.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet