pmbet

Watoto wa chekechea wauawa kwa kisu shuleni nchini Uganda

Eric Buyanza

April 3, 2026
Share :

Nchini Uganda, watoto wanne wamechomwa kisu hadi kufa katika shule moja ya chekechea katika mtaa wa Ggaba nje kidogo ya jijiji kuu Kampala.
 

Polisi wamesema mtuhumiwa wa shambulio hilo Christopher Okello Onyu, mwenye umri wa miaka 34, alijifanya mzazi kabla ya kuanza kutekeleza uhalifu huo.

 

"Mshukiwa anadaiwa kuja hapa siku chache zilizopita akitafuta nafasi kwenye shule hii na akaambiwa arejea tena na akafanya hata kulipa karo ambapo baada ya kufanya hivyo alienda kuwashambulia watoto ambao walikuwa wakicheza kwenye uwanja wa shule na kuwauwa wanne kwa kuwachoma kisu. Watoto waliouwa watatu ni wa kiume na mmoja ni wa kike. Watoto watatu walifariki wakati wakipelekwa hospitalini wakati mwengine akifariki kwenye eneo la tukio." Alisema Rachael Kawala, Msemaji wa Polisi Uganda.

 

Mshukiwa alikamatwa kwenye eneo la tukio na anazuiliwa na maofisa wa polisi. Sababu ya yeye kuteleza shambulio hilo bado haijabainika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet