pmbet

Watoto wa Msuya wagombania Urithi Mahakamani

Sisti Herman

October 23, 2026
Share :

 

Watoto watatu wa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Cleopa Msuya, wapo katika mzozo wa kisheria kuhusu usimamizi wa mirathi yake, huku Mahakama Kuu ikifungua njia kwa ajili ya kusikilizwa kwa maombi yanayolenga kulinda mali za marehemu.

Katika uamuzi uliotolewa tarehe 13 Oktoba 2026, Jaji wa Mahakama Kuu, Sara Mwaipopo, alitupilia mbali pingamizi tano kati ya sita za awali zilizowasilishwa na wasimamizi wa mirathi, John Msuya na Naanjela Msuya, dhidi ya maombi yaliyowasilishwa na ndugu yao, Job Msuya.

Job, akiwakilishwa na wakili Albert Lema, anaomba amri za muda za kulinda mali za mirathi hiyo, akidai kuwa maamuzi yalikuwa yakifanywa bila ridhaa ya pamoja ya wasimamizi. Pia alielezea wasiwasi wake kwamba mali, ikiwemo nyumba iliyopo Upanga, inaweza kuuzwa kwa bei ya chini kuliko thamani yake halisi au kupangishwa kwa masharti yasiyofaa.

Jaji Mwaipopo alikubali kwa sehemu pingamizi moja iliyohusu kasoro katika hati ya kiapo ya Job, na kuamuru kuondolewa kwa aya saba zilizokuwa na maoni, imani binafsi, na hoja za kisheria.

Hata hivyo, Jaji alitupilia mbali hoja za wasimamizi hao kwamba maombi hayo yalikuwa ya haraka mno (hayajakidhi muda mwafaka), hayana msingi wa kisheria, au yamepitwa na wakati, na hivyo kuruhusu shauri hilo la msingi kuendelea kusikilizwa.

Cleopa Msuya, ambaye pia aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Fedha na Waziri wa Viwanda na Biashara, alifariki dunia katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 7 Mei 2025.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet