Watoto wala sumu ya panya wakifikiri ni pipi
Eric Buyanza
April 17, 2024
Share :
Takriban watoto 41 waliwahishwa hospitalini nchini Afrika Kusini baada ya kula sumu ya panya kwa bahati mbaya wakifikiri ni pipi.
Baada ya uchunguzi wa kimatibabu, watoto 17 walilazwa kwa uangalizi maalum huku 24 waliosalia wakiruhusiwa kurudi makwao wakiwa katika hali nzuri.
Mamlaka zimewashauri wazazi na walezi kuchukua tahadhari zaidi ili kuwalinda watoto.