pmbet

Watoto wamshitaki mama yao kwa kuwafukuza nyumbani, kisa kapata Bwana mpya

Eric Buyanza

May 29, 2024
Share :

Huko nchini Kenya watoto watatu wenye umri wa kati ya miaka 11 na 13 wamemfugulia kesi mama yao kwa kuwafukuza nyumbani. 

Inaelezwa kuwa madogo hao walifikia uamuzi wa kumshataki mama yao aitwae Hadja Nabutono mwenye umri wa miaka 43, baada ya mama huyo kuwafukuza nyumbani kwao mwezi Februari baada ya kuolewa na mwanamume mwingine. 

Mbele ya Afisa Mfawidhi wa Wilaya, Collins Kafeero, walidai kuwa mama yao aliwatimua nyumbani na kwenda kuishi na bibi yao. 

Kulingana na gazeti la The Daily Monitor, baba wa watoto hao aliyekuwa mganga wa kienyeji, Sepiriano Omoding, alifariki mwaka wa 2017. 

Kufuatia kifo chake, Mama yao alirithi kipande cha ardhi cha ekari 15 na nyumba. 

Malalamiko ya watoto yalianza wakati mama yao alipoleta mwanamume mpya nyumbani na kuwataka kumwita "Baba".

Kulingana taarifa zilizotolewa na mtoto mkubwa mwenye miaka 13, uhusiano na mama yao ulianza kuwa mbaya alipowashutumu kutomheshimu baba yao wa kambo. 

Watoto hao waliwasilisha kesi kuomba Baba yao wa kambo aondolewe kwenye nyumba ya marehemu Baba yao na kuhakikisha mama yao anawasomesha. 

TUKO

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet