pmbet

Watu 11 wafariki kutokana na hitilafu ya Umeme kiwanda cha Mtibwa Sugar Morogoro

Sisti Herman

May 23, 2024
Share :

Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kuwa watu 11 wamepoteza maisha wakiwemo raia wa kigeni kutokana na hitilafu ya mitambo ya umeme iliyotokea ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar kinachohusika na Uzalishaji wa Sukari.

“Tukio limetokea Saa 7:30 Usiku kuamkia leo Mei 23, 2024, kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme. Waliofariki ni Wataalamu wa Umeme na Mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo”

Amesema kati ya waliofariki kuna Raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil ambapo miili ya wote waliopoteza Maisha imehifadhiwa Hospitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet