pmbet

Watu 116 wafariki kwa kukanyagana kwenye mkusanyiko wa kidini

Eric Buyanza

July 3, 2024
Share :

Mamlaka nchini India, zimesema watu 116 wamefariki katika mkanyagano wakati wa mkusanyiko wa kidini kaskazini mwa nchi hiyo, katika moja ya tukio baya kabisa kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni. 

Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika wilaya ya Hathras kilomita 200 kusini mashariki mwa mji mkuu wa India, New Delhi ambako mkusanyiko mkubwa wa kidini ulikuwa ukiendelea kwenye eneo la wazi. 

Mkusanyiko huo ulikuwa umeitishwa na kiongozi wa kidini kwa ajili ya tamasha la waumini wa Hindu katika kumkumbuka mungu wao wa Shiva.

Matukio kama haya ya mkanyagano yameripotiwa kutokea katika taifa hilo, tukio la karibuni likiwa la Januari 2022 ambapo karibu watu 12 walifariki na wengine kujeruhiwa katika eneo takatifu la Vaishno Devi.

 

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet