pmbet

Watu 14 wakamatwa kwenye maandamano akiwemo Lema.

Joyce Shedrack

September 23, 2024
Share :

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi limewakamata watu 14 wakiwemo mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Lissu na mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini, Godbless Lema.

Kamanda Muliro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa taarifa ya kinachoendelea juu ya maandamano ya maombolezo na amani yaliyoitishwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
 

Muliro amesema watu hao wamekaidi amri halali ya Polisi ya kuacha kushiriki maandamano, jijini Dar es Salaam na wataendelea kuwashikilia kwa ajili ya  mahojiano dhidi yao zaidi.

 

" Jeshi la polisi kanda ya Dar es salaam limekamata watuhumiwa ambao walikuwa wamekaidi agizo la jeshi la polisi ili kutaka kufanya maandamano lakini jeshi la polisi lilishapiga marufuku kwa sababu ambazo jeshi lilizitoa na 14 wapo baadhi ya viongozi hao ikiwemo Freeman Mbowe Tundu Lissu Godbless Lema wamekamatwa pia na wengine waliokuwa wakihamasisha maandamano " amesema Muliro.

pmbet

pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League

pmbet
pmbet