Watu 345 waliopima mkesha wa mwenge wakutwa na VVU
Eric Buyanza
October 16, 2025
Share :
Watu 345 kati ya 62,257 waliojitokeza kupima afya zao kwa hiari katika mikesha ya Mwenge wa Uhuru kwenye halmashauri mbalimbali nchini, wamebainika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), hali inayoonyesha kwamba changamoto ya ugonjwa huo bado ni kubwa.
Takwimu hizo zilitolewa jana jijini Mbeya na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, wakati wa sherehe za kitaifa za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Maadhimisho ya Miaka 26 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Ridhiwani alisema idadi hiyo ya watu waliobainika na maambukizi inawakilisha asilimia 0.6 ya wote waliojitokeza kupima, na kwamba wote walipatiwa ushauri nasaha na kusajiliwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kuanza matibabu.
NIPASHE