Watu 4 wafariki baada ya treni ya abiria kugongana na treni ya mizigo
Eric Buyanza
June 6, 2024
Share :
Takriban watu wanne wamekufa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa wakati treni ya abiria ilipogongana na treni ya mizigo huko Jamhuri ya Czech Jumatano usiku.
Shirika la habari Reuters limeripoti kuwa takriban watu 380 walikuwa wakisafiri kwa treni ya abiria kutoka Prague kwenda jiji la Chop magharibi mwa Ukraine na kugongana na treni ya mizigo iliyokuwa imebeba CARBIDE ya 'Calcium' (kemikali hatari ya viwandani).
Hata hivyo mabehewa mawili ya kwanza yalikuwa tupu, kwa hivyo hakuna uvujaji uliotokea, idara ya zima moto ilisema.
Shughuli za uokoaji zimekamilika na mamlaka zimeahidi kuchunguza ili kujua chanzo cha ajali hiyo.