pmbet

Watu 9 wauawa, 60 wajeruhiwa kwa risasi Marekani

Eric Buyanza

July 21, 2026
Share :

Takriban watu tisa wamepoteza maisha huku zaidi ya wengine 60 wakijeruhiwa kufuatia mashambulizi ya risasi yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini Marekani mwishoni mwa wiki, mamlaka zimesema.
 

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya usalama, mashambulizi hayo yalitokea katika majimbo ya Colorado, Delaware, Maryland, North Carolina, Oklahoma, Arizona, Tennessee pamoja na matukio mawili yaliyorekodiwa katika jimbo la Minnesota.
 

Miongoni mwa matukio hayo, shambulizi moja lilitokea katika maegesho ya mgahawa wa Waffle House uliopo Newark, jimbo la Delaware.

 

Mashambulizi mengine yaliripotiwa kutokea wakati wa sherehe katika mgahawa mmoja uliopo Oklahoma City, nje ya ukumbi wa matukio mjini Minneapolis, pamoja na katika bustani ya umma mjini Jackson, Tennessee.
 

Maafisa wa vyombo vya sheria wamesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha mashambulizi hayo na kuwabaini wahusika waliohusika na matukio hayo.

 

Source: ABC News

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet