Watu 93 wauawa kwenye tamasha la muziki jijini Moscow
Eric Buyanza
March 23, 2024
Share :
Watu zaidi ya 93 wameuawa wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa baada ya watu wenye silaha kumimina risasi kwenye tamasha la muziki jijini Moscow, huku kundi la Islamic State likidai kuhusika imeripoti RFI.
Takriban washambuliaji watano waliokuwa wameficha nyuso zao walifyatua risasi kwa watu waliokuwa wakihudhuria tamasha la muziki wa Rock kwenye ukumbi wa Crocus, ukumbi ambao una uwezo wa kubeba watu 6,200.
Shambulio hilo linatajwa kuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi nchini Urusi tangu kuvamiwa kwa shule ya Beslan mwaka 2004 ambapo zaidi ya watu 330 nusu yao wakiwa watoto waliuawa.
Shambulio hili limekuja ikiwa imepita wiki mbili tangu ubalozi wa Marekani mjini Moscow kutoa tahadhari ya usalama baada ya kupokea ripoti kuwa watu wanaodaiwa kuwa na itikadi kali walikuwa na mipango ya kushambulia mikusanyiko mikubwa mjini Moscow.
Rais Putin hajazungumza hadharani kuhusu shambulio hilo.