Watu watano wafariki kwenye maandamano DRC.
Sisti Herman
June 16, 2024
Share :
Takribani watu watano wamefariki Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika maandamano ya kupinga mauaji ya watu 40 katika kijiji cha Mayikengo Mashariki mwa nchi hiyo.
Mauaji hayo yanatokea baada ya wiki moja kabla watu 80 kupoteza maisha kwa kupigwa risasi na waasi wa ADF wanaopinga serikali ya Rais Yoweri Museveni.
Inashukiwa kuwa kundi la waasi wa ADF ndio wahusika wa mauaji hayo.
Watu hao wamepoteza maisha kutokana na kupigana na walinda usalama ambao walitumia silaha kwa ajili ya kujilinda.