pmbet

Watu wenye silaha washambulia polisi na makanisa huko Dagestan

Eric Buyanza

June 24, 2024
Share :

Watu wenye silaha wameshambulia makanisa mawili ya Orthodox, kituo cha polisi na kuunguza baadhi ya majengo katika Jamhuri ya Dagestan kusini mwa Russia, ambapo Padri na maafisa kadhaa wa polisi wameuawa, shirika la habari la serikali ya Russia, RIA limeripoti.

Video zinaonyesha watu waliovalia nguo nyeusi wakirushia risasi magari ya polisi.

Baada ya shambulio hilo watu hao walikimbia lakini watano kati yao waliuawa na kikosi maalum cha kuzuia ugaidi.

Siku tatu za maombolezo zimetangazwa huko Dagestan, Jamhuri yenye Waislamu wengi kusini mwa Urusi iliyo jirani na Chechnya. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet