pmbet

Watuhumiwa wa shambulio Urusi wafikishwa mahakamani

Sisti Herman

March 25, 2024
Share :

Wanaume wanne waliohusika kwenye shambulizi lililowaua Watu zaidi ya 130 hadi sasa katika eneo la Crocus City Hall Nchini Urusi, wamefikishwa Mahakamani wakikabiliwa na kesi ya ugaidi ambapo wamefikishwa Mahakamani hapo wakiwa na majeraha na muonekano dhaifu unaodaiwa kusababishwa na nguvu iliyotumika kuwadhibiti wakati wa kuwakamata na adhabu ya kuteswa ili wataje waliowatuma na genge lao lote.

Washtakiwa hao wametambuliwa kwa majina ambapo Mshtakiwa wa kwanza anaitwa Dalerdzhon Mirzoyev (32), wa pili Saidakrami Murodali Rachabalizoda (30), wa tatu Shamsidin Fariduni (25) na wanne ni Kijana mdogo Muhammadsobir Fayzov mwenye umri wa miaka 19 ambaye amefikishwa Mahakamani akisukumwa kwenye kiti cha Wagonjwa huku akionekana kuwa mahututi.

Miezoyev na Faridduni na Fayzov wanatajwa kuwa ni Raia wa Tajikistan na mwingine ni Rachabalizoda ambaye uraia wake haujaweka hadharani ambapo wote wamekiri kuwa walihusika na mauaji wakati waliposomewa mashtaka wakiwa ndani ya box la vioo lililowezesha kila Mtu kuwaona.

Kesi imeahirishwa na Washtakiwa wote wanne wataendelea kubaki Mahabusu mpaka watakaporejeshwa Mahakamani May 22,2024.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet