pmbet

Watumishi wa Ardhi msiuze utu kwa vitu vidogo - Pinda

Eric Buyanza

April 10, 2024
Share :

Naibu Waiziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda, amewataka watumishi wa Wizara ya Ardhi kutembea kifua mbele na kuacha kuuza utu wao kwa vitu vidogo vidogo.

Naibu Waziri Pinda amesema hayo Jijini Dodoma, na kuwahimiza watumishi wa sekta ya ardhi kutotoa huduma kwa kuangalia hali za watu na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia haki.

Mhe.Pinda amewakumbusha watumishi hao kufanya kazi kwa utiifu na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwenye vitakatifu na kwa hakika watabarikiwa.

Aidha amewafikishia salamu za pongezi kutoka kwa Rais Samia kwa kupongeza mabadiliko makubwa ya kiutendaji ya Wizara ambapo amewataka watumishi hao kutobweteka ili kuyaishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet