Wauza Mlima kwa shilingi Milioni 20
Eric Buyanza
May 7, 2024
Share :
Jeshi la Polisi wilayani kilosa limewatia mbaroni watu wawili akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msowero A, Petro Sanga (Paroko) mwenzake, Awadh Ngajime kwa tuhuma za kuuza ardhi (eneo la mlima) mali ya kijiji cha Msowero, wilayani Kilosa.
Pia, inaendelea kuwatafuta watu wengine 48 ambao wanaosadikiwa kuwa sehemu ya mtandao uliohusika kuuza kinyume na utaratibu ekari 1158 za Kijiji zilizopo katika mlima huo.
Hayo yalibainika wakati wa mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wanachi katika Kata ya Msowero uliotishwa na Mkuu wa Wilaya ya KIlosa Shaka Hamdu Shaka mwishoni mwa wiki kijjijini hapo.
Shaka amesema kumekuwa na wimbi la uvamizi wa maeneo ya ardhi unaoonekana kukithiri siku hadi siku na baadhi ya maeneo wananchi wamekuwa wakihusika kuyauza kinyume na sheria.
“Mmeuza mlima kinyume na utaratibu ekari 1,158 zote mmevamia na kuuza hii ni mali ya serikali ya kijiji kisha mnageuka kushutumu wengine kumbe wenyewe ndio wahusika, Ocd Huyu mwenyekiti wa kitongoji aliyeshiriki kuratibu mauziano na na kukiri mbele yangu kuwa amelipwa T. shs 500,000 na huyu aliuza eneo la mlima kwa sh 20,000,000 naondoka nao, pia naagiza watu wengine 48 waliohusika kwenye kuuza wajisalimishe vinginevyo watafutwe popote walipo na wafikishwa kwenye vyombo vya sheria,”Amesema.
Shaka pia alipiga marufuku na kuweka zuio la kuendeleza shughuli yoyote katika eneo la mlima unaodaiwa kuuzwa huku akisisitiza kuwa walioziwa maeneo hayo wametapeliwa na mlima huo bado ni mali ya Serikali.
TM