Wazazi wa Jackie Chan, Mama muuza unga, Baba mpelelezi
Sisti Herman
February 2, 2026
Share :

Wazazi wa nguli wa filamu za mapigano, Jackie Chan, wana historia ya kusisimua na yenye changamoto nyingi kama vile filamu zake.
Baba wa Charles Chan, alikuwa akifanya kazi kama mfanyakazi wa ubalozi wa Ufaransa huko Hong Kong, lakini awali alikuwa amehusika katika harakati za kisiasa nchini China na hata kuripotiwa kuwa jasusi wa siri (secret agent) wa serikali ya Nationalist. Alitoroka China kuelekea Hong Kong miaka ya 1940 kukwepa machafuko ya kisiasa.
Mama, Lee-Lee Chan, alifanya kazi kama mfanyakazi wa ndani (housekeeper) na pia alikuwa akijihusisha na biashara ndogondogo, Maisha yake ya awali yalijaa changamoto, Charles Chan alikutana naye alipomkamata (akiwa kama afisa wa forodha) akijaribu kusafirisha dawa za kulevya (opium) ili kupata pesa za kulisha familia yake.
Badala ya kumkamata, alimhurumia na baadaye wakapendana.





