pmbet

Waziri aagiza kukamwatwa kwa aliyeuza eneo la mchina akijua kafa na korona

Eric Buyanza

April 20, 2024
Share :

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ameagiza kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mwanjelwa aliyejulikana kwa jina la Brayan Mwakalukwa na Ezekiel Mwanje mwakilishi wa mmiliki wa anayedaiwa kuuziwa Nyumba ambayo ni mali halali ya Li Shi Cai ambaye ni mwekezaji raia wa China wakidhani amekufa na Korona.
 

Waziri Silaa amaeagiza kutafutwa mtu mwingine mmoja anayefahamika kwa jina la Nida ili aweze kueleza jinsi alivyozibeba milioni 80 ambazo ni pesa za mauzo ya nyumba ya Li Shi Cai.
 

Waziri Silaa ametoa maagizo hayo mapema leo alipotembelea eneo hilo lililopo katika mtaa wa Mwanjelwa jijini Mbeya ili kusikiliza na kutatua mgogoro huo.
 

Watu hao walichukua hatua ya kuuza eneo hilo baada ya kudhani Li Shi Cai amekufa na ugonjwa wa Corona hivyo eneo hilo kukosa mmiliki, wakati mtu alikuwa hai na hakuonekana kutokana na majukumu yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet