Waziri afichua Kabila kutaka kumuua Rais Congo DR
Sisti Herman
June 10, 2025
Share :
Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jean Pierre Bemba, amewashutumu Rais Joseph Kabila, Moise Katumbi na baadhi ya Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki DRC kwa kujaribu kumuua Rais Tshisekedi.
Kabila ambaye alitawala DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019 alikaa siku nyingi mjini Goma ambako alifanya mazungumzo na Makao Makuu ya M23 yanayopinga serikali ya DRC.
Baraza la Maaskofu Katoliki (CENCO) pia limekuwa likitoa wito kwa utawala wa Tshisekedi kufanya mazungumzo na M23 lakini umekataa kusikiliza.
Katika mahojiano na chombo cha habari, Waziri Bemba alisema alikuwa na ukweli wote ambao ulimfanya kuwashutumu watu hao kwa kujaribu kupindua Serikali na kujaribu kumuua Rais Tshisekedi.
Kabila, ambaye alikuwa kimya kwa miaka sita akionekana kuweka siasa kando, alijitokeza tena na kusema anataka kuchangia katika kurejesha nchi hiyo katika amani.