pmbet

Waziri ashuhudia 'Drone' ya utafiti wa madini ikirushwa

Eric Buyanza

February 24, 2024
Share :

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameshuhudia jaribio la urushwaji wa ndege ndogo isiyo na rubani ‘Drone’ kwa ajili ya utafiti wa miamba na madini lililofanyika katika kijiji cha Utimbe kata ya Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Akizunguza katika eneo hilo la utafiti wa madini hususani kinywe, bati, shaba, na chuma, waziri huyo amesema mpaka sasa Tanzania ina taarifa za kina za tafiti wa miamba na madini kwa asilimia 16 zilizopelekea uwepo wa migodi mikubwa ya kati na midogo.

‘’Nchi ikifanyiwa utafiti wa kina wa high resolution airborne geophysical survey wa angalau asilimia 50 ifikapo 2030 itasaidia ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta ya madini.’’amesema Mavunde

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kwa dhati kuhakikisha inawasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia maeneo yenye taarifa za jiolojia ili wachimbe kwa faida na kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet