Waziri Jr afiisha mabao 50 Ligi Kuu
Sisti Herman
April 25, 2024
Share :
Baada ya mshambuliaji wao Waziri Jr kufunga magoli matatu kwenye mchezo wao dhidi ya Tabora United, mabao hayo yalimfanya kufikisha jumla ya mabao 50 tangu ameanza kucheza ligi kuu Tanzania bara maarufu kama NBC Premier League
Katika kumpongeza kwa hatua hiyo kampuni ya INA Sports Brand ambayo ni wazalishaji wa vifaa vya klabu hiyo imemuandalia jezi maalumu ambayo inaonyesha mabao 50 aliyowahi kufunga ndani ya Ligi kuu ya Tanzania.
Hizi hapa Takwimu za Waziri
Toto Afrika- Mechi 13 na mabao 7 (2015-2016)
Toto Afrika- Mechi 17 na mabao 7 (2016-2017)
Azam Fc- Mechi 1 hakuna bao (2017-2018)
Biashara Utd (loan 6 month)- Mechi 6 mabao 3 (2018-2019)
Mbao Fc- Mechi 17 mabao 13 (2019-2020)
Yanga Sc -Mechi 4 mabao 2 (2020-2021)
Dodoma Jiji (6 month)- Mechi 7 mabao 4 (2021-2022)
KMC- Mechi 3 bao moja (2022-2023)
KMC - Mechi 17 mabao 11 (2023-24) na bado msimu unaendelea.
Picha na KMC FC