Waziri Mkuu afutwa kazi baada ya wiki moja
Eric Buyanza
December 21, 2023
Share :
Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco amemfuta kazi Waziri Mkuu, Geraldo Martins wiki moja baada ya kumteua katika nafasi hiyo.
Hata hivyo sababu za kutenguliwa hazikuwekwa wazi, Martins aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu Desemba 12 huu.
Katika taarifa ya utumbuaji na uteuzi iliyosomwa kwenye vyombo vya habari, Rais Sissoco alimteua Rui Duarte de Barros kama Waziri Mkuu mpya.