Waziri Mkuu aliyepo jela apewa tuzo ya Nobel
Sisti Herman
April 1, 2025
Share :
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani Imran Khan aliyefungwa jela, ameteuliwa kuwania tuzo ya amani ya Nobel kutokana na utawala wake na juhudi zake za kutetea haki za Binadamu na Demokrasia.
Tangazo hilo lilitolewa mapema Jumamosi na Wanachama wa Muungano wa Pakistan World Alliance (PWA) kikundi cha utetezi kilichoanzishwa Desemba mwaka jana ambao pia ni wa chama cha siasa cha Norway Partiet Sentrum.
Mnamo mwaka wa 2019, Khan pia aliteuliwa kuwania tuzo ya Amani ya Nobel kwa juhudi zake za kukuza amani huko Asia Kusini.
Januari hii, alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela katika kesi inayohusiana na matumizi mabaya ya mamlaka na ufisadi.
Ilikuwa ni kesi ya nne kuu ambapo Waziri Mkuu huyo wa zamani alipatikana na hatia. Hukumu tatu za awali zinazohusiana na kuuza zawadi za serikali, kuvujisha siri za serikali, na ndoa isiyo halali zilibatilishwa au kusimamishwa na mahakama.
Khan alipoteza mamlaka baada ya kura ya kutokuwa na imani naye Aprili 2022. Alikanusha mashtaka yote dhidi yake, akitaja kuwa yalichochewa kisiasa.