pmbet

Waziri Mkuu awasili Somanga kutekeleza agizo la Rais Samia

Sisti Herman

April 16, 2025
Share :

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mapema leo Jumatano Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua miundombinu ya barabara kuu ya Dar es Salaam-Lindi ambayo imeathiriwa na mvua zinazoendelea nchini.

Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stegomena Tax pamoja na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega.

Mapema jana, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla alisema kuwa Majaliwa atafika eneo hilo kukagua hali halisi na kuhakikisha mawasiliano yanarejea, kama alivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet